JE WAJUA KUWA KISUKARI KINAWEZA KUJIFICHA NA USIJUE KUWA UNACHO.? SOMA HAPA

Makala Hii Ni kwa Msaada wa Mtandao Wa Facebook Na Muandishi Ni Doctor Boaz Mkumbo

Yawezakuwa “Una Kisukari Kilicho Jificha yaani Pre diabetes”.


Kuna Umuhimu wa Kuchunguzwa uwezo wa mwili kutumia
chakula hasa vyakula vya sukari na wanga. Yaani Uchunguzwe
“Insulin Sensitivity” na “Insulin resistance” kwa Kutumia sampuli ya damu yako. Hili litaondoa Utata mwingi wa Kinacho Kusumbua Mwilini na Katika Mfumo wa chakula.
Ugoniwa wa Kisukari sio ugonjwa unaojitokeza gafla. Ni
ugonjwa unaojitengeneza kwa miaka 5-10. Hivyo Ukiambiwa na
daktari Leo sukari iko juu utambue kwamba ugonjwa huo una mizizi ya miaka 5-10. Wengi huwa wana mtazamo Hasi utasikia anajifariji “Ugonjwa huu hata sina siku nyingi ninao, Ni mwezi
jana tu”. Akimaanisha hana haja ya matibabu ya kisukari ya Kimkakati sana kwa sababu ugonjwa bado ni mchanga. La hasha! Siku unatamkiwa Kisukari Ujue Ugonjwa Una Mizizi
Mirefu.
Ugonjwa wa Kisukari ni Ugonjwa wa Ngazi 1-5 na wagonjwa
ambayo hawajitambui kama wana kisukari ni wale ambao wako kwenye Steji ya 1-2 yaani steji ya Utarajiwa kitalamu tunaita
“Pre diabetes” Kisukari Kilicho Jificha.
Mwili unapopungukiwa uwezo wa Kutumia chakula. Mwili
unaanza kutafuta mbinu ya Kujinusuru na hali hiyo ili isiumize
afya yako.
Mfano: Mara tu baada ya Kula sahani ya wali, ndizi, Viazi, Mihogo, Ngano ukashushia na juisi natural kama Embe, Nanasi, tikiti mwili unabaini kuna shehena kubwa ya sukari Inakuja.
Kongosho la Binadamu huzalisha Homoni za Kuratibu Matumizi na mchakato wa chakula mpaka kinafyonzwa. Huzalisha Maji ya Kusaga Chakula (Digestive juice with Enzymes), na Homoni ya Insulin. Sasa kama shehena ya sukari inayokuja kutoka kwenye mfuko wa chakula ni kubwa. Kongosho hutema Homoni ya Kunusuru hiyo sukari isifike kwenye utumbo mwembamba
(Section ya Ufyonzaji). Homoni hiyo huitwa Somatostatin hii Huzuia Kongosho Kutema Homoni za Kukimeng’enya Chakula na huzuia Mfuko wa chakula Usimwage hicho Chakula kwenye Utumbo Mwembamba (Duodenum na Kuendelea).

Lengo la somatostatin ni kunusuru wingi wa Sukari isije
ikafyonzwa yote ikaenda kulemaza mwili. Ni namna mwili
Unavyo Jipambania. Wakati wewe “Unaendelea Kubugia tu
misosi” ukijinadi “Madonda ya Tumbo”
Matokeo ya somatostatin husababisha chakula kuchachuka, Gesi, Kiungulia na tumbo kuwaka moto.
Kwa hiyo basi kama umedumu na Hali hiyo kwa miaka mwaka zaidi ya mmoja. Umetibiwa kwa aina mbalimbali za madawa ya antibiotiki na bado hupati nafuu. Nakushauri Uchunguzwe uwezo wa mili kutumia vyakula na Halafu upangiwe chakula
kulingana na Hatua uliyonayo.
Nimetibu wagonjwa wengi sana waliokuwa tegemezi wa omeprazole, lansoprazole, Heligo Kits baada ya uchunguzi na Kubaini kwamba tatizo lao hata sio “H Pylori” na wala sio
“Vidonda vya Tumbo”. Bali wanasumbuliwa na GERD (Gastro Esophageal Reflux Disease) ambayo Imesababishwa na kupungua kwa uwezo wa mwili Kutumia chakula kwa uharaka.
Unaweza kupima Uchakavu na utendaji wa seli zako kwa
kupima “Insulin sensitivity” na “Insulin resistance” pamoja na
Magonjwa mengine yanayo chakaza seli zako za mwili.

Ni Vizuri pia Kuchunguzwa Choo, Mkojo na Tezi zote za Mwili zinazo ratibu Mfumo wa umeng’enyaji Chakula vizuri.

Ebhana Kama Unasumbuliwa Na Changamoto Hii Basi Usiache Kunitafuta

Unanipata Kupitia Nambari 0747 531 853

Karibu Sana

Leave a Comment