UGONJWA WA KIFUA KIKUU

Makala hii imeandikwa na Doctor Abdul anaepatikana kupitia nambari 0747 531 853

Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na bakteria aitwaye Mycobacterium tuberculosis. Ugonjwa huu hasa huathiri mapafu, ingawa unaweza kuathiri sehemu nyingine za mwili kama vile ubongo, uti wa mgongo, na figo. Ni moja ya magonjwa hatari yanayoweza kusababisha vifo ikiwa hayatachunguzwa na kutibiwa kwa wakati.

Ni nini kifua kikuu

Kifua kikuu ni ugonjwa wa kuambukiza unaoenea kupitia hewa wakati mtu aliyeambukizwa anakohoa, kupiga chafya, au kuongea. Bakteria hao wanaweza kubaki hewani kwa muda na kuambukiza watu wengine ambao wanapumua hewa hiyo.

Dalili za Kifua Kikuu

Dalili za kifua kikuu zinaweza kutofautiana kulingana na eneo ambalo ugonjwa huo umepiga. Hata hivyo, dalili kuu ni pamoja na:

  • Kikohozi kikali kinachoendelea kwa zaidi ya wiki mbili.
  • Kutokwa na damu au kamasi yenye damu wakati wa kukohoa.
  • Maumivu ya kifua.
  • Homa na joto la mwili linaloendelea.
  • Kupungua kwa uzito bila sababu ya msingi.
  • Uchovu wa kudumu.
  • Kutokwa jasho usiku.

Sababu za Kifua Kikuu

Ugonjwa huu unasababishwa na bakteria wa Mycobacterium tuberculosis. Ugonjwa huo huenea wakati mtu aliyeambukizwa anaweza kutoa bakteria hawa kwenye hewa kwa njia ya kikohozi au chafya, na watu wengine wanapopumua hewa hiyo, wanaweza kuambukizwa.

Watu Walio Hatarini Kupata Kifua Kikuu

Kuna makundi kadhaa ya watu walio hatarini zaidi kupata kifua kikuu, ikiwa ni pamoja na:

  • Watu walio na kinga ya mwili iliyopungua kutokana na VVU/UKIMWI au magonjwa mengine ya kinga ya mwili.
  • Watu wanaoishi katika maeneo yenye viwango vya juu vya maambukizi ya kifua kikuu.
  • Watu wanaotumia dawa za kudhibiti kinga ya mwili.
  • Watoto na wazee wenye kinga duni.

Madhara ya Kifua Kikuu

Madhara ya kifua kikuu yanaweza kuwa makubwa, hasa ikiwa hayatatibiwa kwa wakati. Madhara yanaweza kujumuisha:

  • Uharibifu wa mapafu au sehemu nyingine za mwili.
  • Kusababisha vifo ikiwa hayatatibiwa.
  • Maambukizi ya kifua kikuu sugu ambayo yanaweza kuwa magumu kutibu.

Tiba ya Kifua Kikuu

Tiba ya kifua kikuu inahusisha matumizi ya dawa za antibiotics. Marra nyingi matibabu huchukua muda wa miezi 6 hadi 9, kulingana na hali ya mgonjwa. Ni muhimu kumaliza dozi kamili ya matibabu ili kuhakikisha bakteria wote wanauawa na kuepusha maendeleo ya aina sugu za ugonjwa huu.

  • Matibabu ya kawaida ni pamoja na dawa kama isoniazid, rifampin, ethambutol, na pyrazinamide.
  • Kwa maambukizi sugu, tiba inaweza kuwa na dawa za ziada na inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.

Umuhimu wa kutumia tiba lishe na dawa za hospital kwa pomoja wakati wa kutibu Kifua Kikuu.

Watu wengi wameacha dozi ya kifua kikuu kwa sababu dozi yake ni ya muda mrefu na wanajiona kuwa wapo vizuri kiafya hawana haja ya kuendelea na tiba.

Kwanza si mshauri mtu kuacha dozi yake yoyote ile hata kama utatumia tiba lishe endelea na dawa yako mpaka utakapomaliza dozi yako.

Sasa tukirudi upande wa tiba lishe ni kwamba ukitumia tiba lishe itakupa nguvu zaidi na afya iliyobora zaidi hivyo wewe utakuwa tofauti na wagonjwa wengine.

Hivyo ni muhimu kwako kitumia tiba hizi maana pia itakusaidia kupona haraka zaidi bila hata ya kupata uchovu na madhara mengine yatokanayo na ugonjwa.

Unaweza kunipigia Leo kupitia nambari 0747 531 853 ili tuweze kujadiliana kuhusu afya yako na namna za wewe kupata afya iliyo imarika katika kila sekta.

Karibu sana

Leave a Comment