Makala hii imeandikwa na Doctor Abdul anaepatikana kupitia nambari 0747 531 853

Nchini Ujerumani, matumizi ya bangi kwa madhumuni ya burudani yaliruhusiwa mwaka 2023. Sheria hii inaruhusu watu wazima wenye umri wa miaka 18 na zaidi kununua na kutumia bangi kwa kiwango kidogo, hadi gramu 25 kwa siku na jumla ya gramu 50 kwa mwezi. Pia, sheria inaruhusu upandaji wa mimea ya bangi nyumbani kwa madhumuni ya kibinafsi, hadi mimea 3 kwa mtu mmoja.
Faida za Bangi
1. Kutuliza Maumivu: Bangi inaweza kusaidia kutuliza maumivu sugu na yenye nguvu kwa baadhi ya wagonjwa.
2. Kudhibiti Magonjwa: Imethibitika kuwa bangi inaweza kusaidia kudhibiti magonjwa kama vile kifafa na magonjwa ya kunyoosha misuli.
3. Kupunguza Wasiwasi: Kwa kiwango kidogo, bangi inaweza kusaidia watu kupunguza wasiwasi na stress.
4. Kuongeza Hamu ya Chakula: Kwa watu wenye matatizo ya lishe, bangi inaweza kusaidia kuongeza hamu ya kula.
Maadhara ya Bangi kwenye Mwili wa Binadamu
1. Athari kwenye Mfumo wa Fahamu: Bangi inaweza kuathiri ubongo na mfumo wa fahamu, hasa kwa vijana.
2. Kuharibu Kumbukumbu: Matumizi ya bangi yanaweza kusababisha kupoteza kumbukumbu, hasa kwa matumizi ya muda mrefu.
3. Kulevya: Bangi inaweza kusababisha utegemezi kwa baadhi ya watu, na hivyo ni muhimu kutumia kwa kiasi.
4. Kushusha Ufahamu: Matumizi ya bangi yanaweza kupunguza uwezo wa kuzingatia na kufikiria kwa umakini.
Ushauri kwa vijana Kuhusiana na Matumizi ya Bangi
Hapa kwetu bangi imeonyesha kuwa ina madhara zaidi kuliko faida hivyo ni bora kuepukana nayo kabisa.
Na inawezekana aina ya bangi inayolimwa hapa kwetu haina viwango vizuri kwa matumizi ya binadam hivyo ni bora kujiepusha nayo kwani inaweza kukuletea madhara makubwa kuliko faida
Lakini pia hata huko Ujerumani matumizi ya bangi yameruhusiwa kwa kiwango kidogo sana.