Ugonjwa wa Stroke: Kielelezo cha Tishio kwa Afya ya Moyo

Ugonjwa wa stroke, unaojulikana kama kiharusi kwa lugha ya kawaida, ni tishio kubwa kwa afya ya moyo na ubongo. Huathiri mamilioni ya watu kila mwaka ulimwenguni kote na unaweza kuwa na athari kubwa kwa maisha ya mtu binafsi na familia zao. Makala hii inalenga kuchambua maana ya ugonjwa wa stroke, sababu zake, dalili zake, watu walio hatarini kupata stroke, na tiba zake.

Maana ya Stroke

Stroke hutokea wakati usambazaji wa damu kwenye sehemu ya ubongo unakatizwa au kuna uvujaji wa damu ndani ya ubongo. Hii husababisha kifo cha seli za ubongo na mara nyingi huacha athari za kudumu kama vile upotevu wa uwezo wa kusema, kutembea, au kufanya shughuli za kila siku.

Sababu zinazopelekea stroke kutokea:

Sababu za kawaida za stroke ni pamoja na

  • shinikizo la damu (pressure)
  • uvutaji sigara
  • kisukari
  • unene kupita kiasi
  • lishe duni
  • mlo wenye mafuta mengi
  • kutofanya mazoezi ya kutosha
  • historia ya familia ya ugonjwa wa moyo na mzunguko wa damu inaweza kuongeza hatari ya mtu kupata stroke.

Dalili za Stroke

Dalili za kawaida za stroke ni pamoja na;

  • upotevu wa nguvu upande mmoja wa mwili
  • kigugumizi
  • upofu au upungufu wa maono
  • kizunguzungu
  • kichwa kuuma.

Wahi hospital unapoana hizi dalili maana uwahi kupata tiba kabla tatizo halijawa kubwa na kupelekea uharibifu mkubwa kwenye ubongo

Watu Walio Hatarini kupata stroke

Watu walio katika hatari kubwa ya kupata stroke ni pamoja na wazee, watu wenye mlo mbaya, walio na historia ya matatizo ya moyo au mzunguko wa damu, na wale ambao hawafanyi mazoezi ya kutosha.

Tiba za Stroke

Tiba za stroke zinaweza kujumuisha dawa za kupunguza damu, upasuaji kurekebisha mishipa ya damu, na mabadiliko ya mtindo wa maisha kama vile lishe bora na mazoezi ya mara kwa mara. Programu za ukarabati wa ubongo zinaweza pia kusaidia wagonjwa kuwarejesha kwenye hali yao ya kawaida au kupunguza athari za uharibifu wa ubongo.

Na kwa wale ambao wanaonyesha dalili za ugonjwa huu ni muhimu ukawahi kupata tiba na bora ukawahi hospital sio ujaribu kujitibu mwenyewe nyumbani kwako.

Pia ningependa kukukaribisha kwenye clinic yetu ya tiba lishe ili uweze kutibiwa tatizo hili na matatizo mengine yote yanayo husu afya ya mwanadamu kwa kutumia mimea tiba na tiba za asili vilivyopo kwenye mfumo wa vidonge, unga, kahawa na majani ya chai.

Kwanini utumie Tiba lishe ama tiba mbadala.??

Kwa sababu tiba lishe haina kemikali nyingi kama tiba za hospitalini hivyo kuupa mwili wako tiba tu na sio uchafu wa kemikali lakini pia tiba hizi zina matokeo ya haraka na ya kudumu lakini pia tiba hizi zinatibu matatizo mengi sana yaani dawa moja inaondoa matatizo hata 6 na zaidi na pia husafisha na kuondoa sumu zote mwilini.

Wasiliana nasi kupitia nambari 0747 531 853 au fika ofisin kwetu Dar es salaam Kariakoo

Leave a Comment