MARADHI YA MOYO

Makala hii imeandikwa na Doctor Abdul anaepatikana kupitia nambari 0747 531 853

Maradhi ya moyo ni moja ya tatizo kuu linalo athiri watu wengi duniani. Maradhi haya hushambulia mshipa mkuu unao rudisha damu kwenye moyo.

Mafuta yanayo gandia kwenye mishipa ya damu (cholesterol deposits) ndio chanzo kikuu cha maradhi ya moyo kwa maana moyo utatumia nguvu kubwa kusukuma kiwango kidogo cha damu na hii ikiendelea kwa muda mrefu moyo huanza kupata hitilafu.

Dalili za maradhi haya hutofautiana kati ya wanaume na wanawake. Kwa mfano wanaume, hupata maumivu ya kifua na wanawake wanaweza kuonyesha dalali za ziada lakini pia kuhisi kichefuchefu, kushindwa kupumua vizuri na uchovu wa hali Ya juu.

DALILI ZA MARADHI YA MOYO

Maumivu ya kifua, kifua kubana, mapigo ya moyo kwenda mbio na kuhisi maumivu ndani ya kifua (kwenye moyo)

Kushindwa kupumua vizuri

Maumivu ndani ya shingo, kwenye koo, pia kwenye taya na maumivu ya tumbo karibu kabisa na kifua (chembe).

Maumivu ya miguu, ganzi za miguu, au kuhisi ubaridi kwenye miguu au mikono

Dalili nyingine za maradhi ya moyo ni;

Miguu kuvimba

Mtu kuwa wa blue hasa kwenye viganja vya mikono

Kizunguzungu

Maumivu ya kichwa na kichwa kuwa kizito

Kuzimia

Mapigo ya moyo kwenda kasi

Mapigo ya moyo kwenda kidogokidogo sana

Mwili kuishiwa nguvu mara kwa mara

Uchovu uliopitiliza

Mwili kuvimba au baadhi ya viungo kuvimba hasa miguu na mikono

Kukohoa kikohozi kikavu

Homa

Kukohoa kwa muda mrefu

Ngozi kupata vipele na vidoa vya ajabu

NI MUDA GANI WA KUMUONA DAKTARI

Wahi hospital ukianza kuona dalili hizi;

Maumivu ya kifua

Kukosa pumzi/kushindwa kupumua vizuri

Kuzimia ghafla. (Huumwi ila ghafla unapoteza nguvu na unazimia)

NINI KINASABABISHA MARADHI HAYA

Ili tuweze kujua nini kinasababisha maradhi haya ni lazima tujue aina ya maradhi ya moyo kwa sababu kuna aina tofauti ya maradhi ya moyo.

Hivyo ni lazima kujua namna gani moyo unafanya kazi.

  • Moyo umegawanyika katika vyumba Vinne. Vyumba viwili juu vinavyoitwa Atria na vyumba viwili vya chini vinavyo itwa Ventricles
  • Upande wa kulia wa moyo hupeleka damu kwenye mapafu kupitia mishipa ya pulmonary Artery
  • Ndani ya mapafu, damu huchukua hewa safi (oxygen) kisha hurudi kwenye moyo kwa upande wa kushoto kupitia vein za pulmonary
  • Kisha upande wa kushoto wa moyo husukuma damu kupitia mshipa wa Aorta kwenda kwenye viungo vya mwili mzima

VALVE ZA MOYO

Moyo una valve nne au tuseme komeo au kufuli nne. Hizi komeo hufunga pale tu inapohitajika kufunga na hufunga kwa kukaza kwelikweli ili kuepesha kuvuja

MAPIGO YA MOYO

Moyo hufanya kazi kwa kujibana na kisha una relax na kila tukio lina maana. Moyo ukijibana vyumba vya chini hujikusanya mahala pamoja hivyo kupelekea damu kusambazwa kwenye mapafu na mwili mzima. Na kipindi moyo umerelax basi damu huruhusiwa kuingia tena ndani ya moyo.

MFUMO WA UMEME KWENYE MOYO

Mfumo wa umeme ndio hufanya moyo kuendelea kupiga. Mapigo ya moyo ndio yanayo wezesha zoezi mabadilishano ya damu yenye oxygen na damu ambayo bado haina oxygen.

Mabadilishano haya ya damu yenye oxygen na damu isiyo na oxygen ndio inatufanya tuweze kuendelea kuishi.

SASA TURUDI KWENYE MADA YETU NINI KINACHOSABABISHA MARADHI YA MOYO

Sababu kuu ya maradhi haya ni mafuta mabaya au mafuta mengi kuzunguka kwenye mishipa ya damu (ndani ya mishipa mafuta hutanda pembezoni mwa mishipa hivyo kufanya mshipa kuwa na mafuta yasiyo na kazi). Na swala hili huchangiwa sana na;

  • Mlo mbovu, chakula chenye mafuta mengi na kutozingatia ulaji sahihi
  • Kutokufanya mazoezi, mazoezi mepesi sana kama vile kutembea na kuruka kamba inaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kujikinga na maradhi haya
  • Unene uliopitiliza
  • Unywaji pombe uliopitiliza na uvutaji sigara
  • Ulaji wa vitu venye sukari nyingi sana mara kwa mara
  • Kuongeza chumvi kwenye chakula kikiwa tayari mezani.

WATU GANI WAPO HATARINI KUPATA MARADHI HAYA.

Watu walio hatarini kupata maradhi ya moyo ni pamoja na;

  • Umri, watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 40 na kuendelea wapo hatarini zaidi kupata maradhi haya kuliko vijana wadogo. Lakini haimanishi kuwa vijana wadogo hawawezi kupata ugonjwa huu
  • Jinsia, wanaume wapo hatarini zaidi kupata changamoto hii kuliko wanawake. wanawake wanakuwa hatarini baada ya ukomo wa hedhi lakini pia wanawake wanaweza kupata tatizo hili muda wowote
  • Historia ya ugonjwa huu ndani ya familia, kama kwenu mna matatizo ya maradhi haya basi ni rahisi sana kuupata ugonjwa huu
  • Wavuta sigara, kama wewe ni mvutaji sigara acha kwa maana kwenye tumbaku kuna viambata vinavyo chochea uharibifu wa mishipa ya damu
  • Ulaji mbovu, vyakula vyenye sukari nyingi, chumvi nyingi na mafuta mengi ni hatari kwa afya ya mishipa yako hivyo jitahidi kula vyakula vyenye faida na mwili wako
  • Wagonjwa wa kisukari, kisukari na maradhi ya moyo ni magonjwa yanayo kwenda sambamba mara nyingi mwenye kisukari hupata maradhi ya moyo na mwenye maradhi ya moyo hupata kisukari
  • Kutokufanya mazoezi kabisa, mazoezi husaidia kuyeyusha mafuta mabaya mwilini na kama hufanyi kabisa mazoezi na kazi zako ni za Ofisin tu na Ofisin pia kuna air-conditioning hutoki hata jasho upo kwenye hatari kubwa
  • Kuwa na mawazo yaliokithiri (stress), msongo wa mawazo unawasumbua watu wengi sana na hata hivi sasa vijana wadogo wanapata maradhi haya kwa sababu ya msongo wa mawazo.  Epuka kukaa na watu wenye mtazamo mbaya na vilevile ishi kwa kumtegemea muumba wako acha kujipa mizigo isiyo yako.

JE NAWEZA KUPATA TIBA YA MARADHI HAYA

Maradhi haya yanatibika tena kwa njia tofautitofauti njia ya kwanza ni kwenda hospital na kupewa tiba kulingana na majibu ambayo utapatiwa na hospital kama itakuwa ni upasuaji au njia ya vidonge na sindano.

Na njia ya pili ni kufika kwenye kituo cha tiba lishe chochote ili uweze kupata tiba. Mimi ni daktari ila napendelea zaidi kutumia dawa za tiba lishe kwa wagonjwa wangu kwa sababu dawa hizi hazina kemikali na pia zinamatokeo ya haraka na pia zinaondoa tatizo kwa kiasi kikubwa bila ya kurudia rudia dozi.

Kwa mahitaji ya tiba zetu mbadala au tiba lishe zenye uhakika na ubora zaidi wasiliana nasi kupitia nambari 0747 531 853

Leave a Comment