SUMU ZA MWILINI NA JINSI YA KUZIONDOA

Makala hii imeandikwa na Doctor Abdul utampata kupitia nambari 0747 531 853

Kwanza tuanze kwa kuzifahamu sumu za mwilini na zinatoka wapi.

Sumu zinaingia mwilini mwetu kwa njia ya mdomo (kuzinywa/kula) pia kwa njia ya hewa (kuvuta hewa chafu).

Na mara nyingi tunaingiza hizi sumu mwilini bila ya sisi wenyewe kujua. Na hii ni kutokana na mazingira ya maisha yetu ya kila siku.

Sumu nyingi tunaipata kwenye vyakula vyetu vya kila siku na vilevile dawa tunazokunywa kila siku. Nyingine ni zile sumu zinazozalishwa na viwanda ama vyombo vya usafiri hii ni sumu iliyo kwenye mfumo wa gesi hivyo tunaivuta bila ya sisi kujua.

SUMU ZITOKANAZO NA DAWA

Kila dawa unayotumia kutibu ugonjwa flani ina kiwango flani cha takataka na vilevile inasababisha kero ndogondogo (side effects).

Hizi dawa hazitakiwi kutumika kwa muda kwani zinamadhara makubwa kama zikitumika kwa muda mrefu. Lakini vilevile kwa kiasi kikubwa bado hatujajua madhara ya muda mrefu yatokanayo na kemikali zinazotengezewa hizi dawa.

Pia kwa wale wenye tabia ya kujiandikia dawa bila kufata masharti wala kupima hili ni jambo la hatari sana.

Madhara yatokanayo na matumizi ya dawa flani kwa muda mrefu yapo mengi na pia tunawaona wagonjwa wanaokuja hospital kila siku. Hivyo ni muhimu kupunguza Matumizi yasiyo ya lazima ya dawa.

VYAKULA

Vyakula vingi tunavyokula havina faida na miili yetu kwa sababu ya aina ya upishi wa vyakula hivyo. Lakini pia ulaji usio sahihi wa vyakula.

Kwa mfano haifai mtu kuchanganya matunda tofautitofauti kwenye sahani moja na kuyala pamoja kama vile ambavyo haifai kula chakula pamoja na matunda ndani ya muda mmoja.

Pia kula chakula na kunywa maji ama soda ama juisi kwa muda mmoja, hii haina faida yoyote kiafya na zaidi inaupa mwili kazi kubwa sana na baada tu ya kufanya hivyo unaanza kuhisi mwili umekuwa mzito na unajisikia usingizi tu.

SUMU ZA VIWANDANI

Hizi ni sumu zitokanazo na hewa chafu iliosambaa, ama moshi wa vyombo vyetu vya usafiri, moshi wa aina Yoyote tunaouvuta kwa makusudi ama kwa bahati mbaya.

Na kwa sababu za dunia kupiga hatua kila siku viwanda vipya vinafunguliwa na hivyo tunazidi kuhatarisha maisha yetu.

Njia ya kujikinga na hewa chafu ni kwa kuva barakoa (mask) kwa ajili ya kutulinda na hewa chafu.

NINI HUTOKEA SUMU ZIKIINGIA MWILINI

Baada tu ya sumu kuingia mwilini mtu hatoona dalili zozote za shida yoyote kwa sababu sumu hizi hukaa mwilini kwa muda mrefu sana lakini pia sumu hizi huvamia seli kwa kipindi flani.

Sumu hizi huge hugeuka na kuwa Radikali huru (free radicals), hizi radikali ndizo husababisha kanza kwa baadhi ya watu lakini pia husababisha matatizo ya ngozi kama vile ngozi kusinyaa na kupoteza mvuto.

Pia hizi radikali ni hatari sana kwani huweza kuvamia mfumo wa kinga na kumfanya mtu kuwa dhoofu kila wakati na kuwa mnyonge.

Radikali hizi zikiwa nyingi huweza kusababisha kansa ya eneo lolote kwenye mwili wa binadam.

NINI CHA KUFANYA

Wengi wetu ni wahanga wa free radicals japo wengi bado hatujajua.

Hivyo cha kufanya ni kuziondoa sumu hizi kupitia kwa njia ya kutoa sumu aidha kwa kufanya chuku/hijama ama kwa kutumia tiba lishe (vidonge maalum visivyo na kemikali) zinazotoa sumu hizi.

Kumbukumbu sumu ikishaingia mwilini haina uwezo wa kujitoa yenyewe ni mpaka itolewe hivyo ni muhimu ukawahi mapema kucheki afya yako.

Kwa mwenye uhitaji wa tiba hizi wasiliana nasi kupitia nambari 0747 531 853

Karibu sana

Leave a Comment