
Ugonjwa wa pelvic inflammatory disease (PID) ni ugonjwa ambao huathiri viungo vya uzazi kwa wanawake, ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ya zinaa.
Ugonjwa huu mara nyingi huwakumba wale wanawake wanao shiriki ngono na wanaume zaidi ya wawili yaani mtu mwenye wapenzi wengi tena bila ya kutumia kinga.
Tafiti zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 5 ya wanawake wanao ugonjwa huu.
Walio hatarini kupata PID ni Wafuatao:
Watu walio hatarini zaidi ni wale wenye magonjwa ya zinaa kama vile kaswende na kisonono au ambae alishawahi kupata maambukizi ya magonjwa haya. Japokuwa unaweza kupata PID bila ya kuwa na magonjwa haya.
Walio hatarini kupata PID ni;
● wanawake wenye wapenzi wengi
● kufanya mapenzi bila kutumia kinga
● waliotoka kufasafishwa kizazi kwa kutumia vifaa
● walio wahi kuwa na ugonjwa huu hapo nyuma
Dalili za PID
Baadhi ya wanawake wenye PID hawaonyeshi dalili zozote na wala hawajijui kama wana tatizo hili. Ila sio wote ambao hawataonyesha dalili wengine wataonyesha dalili zifuatazo;
● Maumivu chini ya kitovu
● Homa
● Maumivu wakati wa kufanya mapenzi
● Maumivu wakat wa kujisaidia haja ndogo
● Hedhi isiyokuwa na mpangilio maalum
● Kutokwa na majimaji yenye harufu mbaya ukeni
● Mwili kuchoka na kuishiwa na nguvu
● Maumivu ya tumbo kwa baadhi ya watu
NINI TIBA YA PID
PID hutibiwa kwa kutumia antibiotics maana ugonjwa huu ni wa bacteria hivyo magonjwa yote ya bacteria hutibiwa kwa kutumia antibiotics.
Ndani ya muda mchache wa kuanza kutumia dawa utaona mabadiliko pia ni lazima umalize dose hata Kama unajiona umepona. Na pia kipindi upo kwenye dose jiepushe kufanya mapenzi.
Kwa wale ambao kinga zao za mwili zimeshuka hivyo kupelekea kuchelewa kupona basi anaweza kutumia tiba lishe au virutubisho vinavyo uzwa na makampuni tofaut ili uweze kuongeza kinga yako.
Muandishi
Niite Doctor Abdul, daktari mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitano kwenye sekta hii ya Afya, pia nimehudumia maelfu ya wagonjwa na nimekuwa sababu ya maelfu ya watu kupona matatizo yao.
Kwa sasa nimejikita kwenye Tiba Lishe au Tiba Mbadala kwa sababu nimeona wagonjwa wengi wakipona kupitia Tiba hizi na hata Wagonjwa Wangu walio tumia Tiba hizi wamerudisha Mrejesho unao ridhisha Sana.
Unanipata kupitia Nambari 0747 531 853.
Karibu Sana