
Tarehe 10 ya mwezi huu Justin Beiber aliwashangaza mashabiki wake wengi baada ya kupost video kwenye mtandao wa Instagram akithibitisha kuwa amepatwa na tatizo la kuparalaiz upande mmoja wa uso wake.
Justin amesema alipimwa akakutwa na ugonjwa unaoitwa RAMSAY HUNT SYNDROME ugonjwa ambao ni nadra sana kuwapata watu. Ugonjwa huu hutokea pale ambapo vipele aina ya shingles vinapo shambulia mfumo wa neva wa usoni. ( Shingles inapovamia uso).
Ugonjwa huu una sababishwa na virusi wanaotoka familia moja na wanaosababisha maradhi kama matetekuwanga na ugonjwa maarufu wa ngozi unaojulikana kama mkanda wa jeshi.
Kwenye video aliyoipost Instagram msanii huyu anaonekana hawezi kutumia upande mmoja wa uso wake kabisa hata kucheka anacheka upande mmoja.
Haijulikani ni lini alikutwa na ugonjwa wa RAMSAY HUNT SYNDROME. Ila taarifa zilitoka mda mchache baada ya msanii huyu kuahirisha matamasha yake ya mwaka huu 2022 Justice world tour kwa sababu ya maradhi ambayo hayakutajwa
JE NINI MAANA YA RAMSAY HUNT SYNDROME (RHS)
Ugonjwa wa RHS humpata mtu pale ambapo vipele (shingles) vinapo shambulia maeneo ya uso karibu na moja ya sikio lako. Ugonjwa huu husababisha maumivu makali pamoja na uso kuparalaiz na kushindwa kusikia upande ambao pigo hili limetokea.
Ugonjwa huu ambao kwa mara Ya kwanza uligundulika mwaka 1907 na daktari Ramsay Hunt, Huwapata watu wenye virusi vya maradhi ya ngozi kama vile mkanda wa jeshi, virusi wanao sababisha shingles na matetekuwanga hivyo watu ambao wana maradhi haya wapo kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.
Hata hivyo taarifa nzuri ni kwamba ugonjwa huu ni nadra sana kwenye kila watu 100,000 basi watu wa 5 tu ndio waneweza kuwa nao.
RHS husababisha kipele chenye maumivu kwa nje Ya sikio na kwa ndani kidogo ya sikio na maumivu makali sana ya sikio kwa ujumla na watu wengi hupata tatizo la kuparalaiz uso.
Kama tatizo hili halitotibiwa ndani Ya siku 3 inaweza kupelekea mtu kupata uziwi wa moja kwa moja pia matatizo ya kuparalaiz uso moja kwa moja.
Ugonjwa huu hutibiwa kwa mgonjwa kupewa dawa zinazo pambana na virusi ( anti virus) kama vile acyclovir na famciclovir pia mgonjwa hupewa dawa za kuondoa uvimbe (anti inflammatory).