0747 531 853

Chunusi ni moja ya changamoto kubwa sana duniani, inakadiriwa kuwa huathiri asilimia 85 ya vijana wadogo.
Chanzo kamili cha chunusi bado hakijulikani isipokuwa chunusi zinahusishwa sana na;
●Stress
●Mabadiliko ya hormone mwilini
●Genetics (kurithi)
●Aina flani ya vyakula
Tiba nyingi maarufu za hospital za chunusi kama vile salicylic acids, niacinamide, au benzoyl peroxide huwa zinasaidia sana isipokuwa gharama zake ni kubwa na pia huleta madhara mengine kama ngozi kuwa kavu sana, kutengeneza wekundu katika ngozi na pia ngozi kuwasha kwa baadhi ya watu.
Hii imepelekea kuwafanya watu wengi kujaribu kujitibu chunusi kwa njia asilia.
NJIA SAHIHI ZA ASILI ZA KUONDOA CHUNUSI
1 Apple cider vinegar (siki ya apple)

Hii vinegar tafiti zinaonyesha kuwa ina uwezo mkubwa wa kupambana na bacteria wa aina nyingi pamoja na fangasi wa aina tofaut
JINSI YA KUTUMIA 1. Chukua kijiko kimoja kikubwa cha vinegar changanya na glass moja ya maji 2. Baada ya kuosha uso wako kwa maji safi na Sabuni tumia mchanganyiko huu wa vinegar na maji kujipaka usoni. 3. Iache ibaki usoni kwa muda wa dakika moja kisha suudha uso wako. 4. Paka mara mbili kwa siku asubuh na jioni
Vinegar ina asili ya ukali hivyo tumia vinegar kidogo changanya na maji mengi ili isikubabue uso ama sehem nyingine unapo taka kuipaka
2. Tengeneza mask ya kitunguu swaum na asali
Tafiti zilizofanyika 2017 zilionyesha kuwa mchanganyiko wa asali na swaum vilisaidia sana kuondoa chunusi pia mchanganyiko huu ulionyesha uimara wake zidi ya bacteria na pia huondoa sumu mwilini. Kwa kifupi mchanganyiko huu una faida nyingi sana
JINSI YA KUTUMIA 1. Chukua asali vijiko viwili vikubwa changanya na swaum iliyopondwa nusu kijiko kidogo. 2. Baada ya kuwa umeuosha uso wako vizuri paka mchanganyiko huu kisha uache kwa dakika 15. 3. Baada ya dakika 15 safisha uso wako kwa maji baridi na ufute kabisa uache uso ubaki mkavu kabisa.
3. TUMIA ALOE VERA (SHUBIRI)

Aloe Vera inajulikana kwa kuwa tiba kwa maradhi mengi pia faida zake nyingi zinajulikana duniani kote. Aloe Vera kulingana na tafiti hutumika kutibu matatizo ya ngozi kama vile muwasho, ngozi iliyoungua ama kubabuka, pia hutumika kutibu vidonda
JINSI YA KUTUMIA 1. Kamua majimaji ya aloe Vera kwa kutumia njia Yoyote utakayoweza 2. Tumia maji hayo bila kuchanganya na kitu kingine kujioshea usoni. 3. Jikoshee maji haya asubuh na jioni mpaka utakapo pata matokeo
Njia asilia zipo nyingi sana ila hizi nilizokuletea ndio rahisi zaidi na ndio zilizofanunyiwa tafiti nyingi zaidi duniani
Usisite kuweka comment yako na kushare post hii ili uwanufaishe na wengine wenye tatizo hili
Pia kwa wewe ambae umejaribu nyingi na bado hujapata matokeo nitafute kupitia nambari 0747 531 853 ili niweze kukupatia suluhisho la kudum kwa gharama nafuu kabisa